Mark 10:1-6

Mafundisho Kuhusu Talaka

(Mathayo 19:1-12; Luka 16:18)

1 aIsa akaondoka huko, akavuka Mto Yordani, akaenda sehemu za Uyahudi. Umati mkubwa wa watu ukaenda kwake tena, naye kama ilivyokuwa desturi yake, akawafundisha.

2 bBaadhi ya Mafarisayo wakaja ili kumjaribu kwa kumuuliza, “Je, ni halali mtu kumwacha mke wake?”

3Isa akawajibu, “Je, Musa aliwaamuru nini?”

4 cWakajibu, “Musa aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.”

5 dIsa akawaambia, “Musa aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. 6 eLakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke.
Copyright information for SwhKC